Hotel Center by Google

Sheria na Masharti

 

Sheria na Masharti haya ya Hotel Center by Google (“Masharti”) yanakubalianwa kati ya Google Ireland Limited (“Google”) na huluki inayotekeleza Masharti haya au inayokubali Masharti haya kielektroniki (“Mshirika wa Safari za Google”).  Masharti haya yanadhibiti jinsi Mshirika wa Safari za Google anavyotumia Google Hotel Center, ikiwa ni pamoja na huduma husika, vipengele na sifa (“Huduma”) (i) zinazoweza kufikiwa kupitia akaunti moja au zaidi zilizotolewa kwa Mshirika wa Safari za Google kuhusiana na Masharti haya (“Akaunti”) au (ii) zinazojumuisha Masharti haya kwa kurejelea (kwa pamoja “Hotel Center”). 

 

1. Kutumia Hotel Center.  Mshirika wa Safari za Google anaweza kuwasilisha data, mipasho au maudhui mengine (“Maudhui”) kwa Hotel Center kwa kutumia mbinu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutumia API za Google. Mshirika wa Safari za Google anakubali kuwasilisha Maudhui kwa njia ambayo inatii maagizo au vipimo vyovyote vilivyotolewa na Google kwa Mshirika wa Safari za Google. Google inaweza kutoa utendakazi unaomruhusu Mshirika wa Safari za Google kutoa, kuunganisha, kuhamisha au kutumia vinginevyo Maudhui kutoka kwenye Hotel Center kwa kutumia huduma nyingine ya Google. Katika hali hiyo, sheria na masharti ya huduma hiyo nyingine ya Google yatatumika kuhusiana na jinsi Mshirika wa Safari za Google anavyotimia huduma hiyo, ilmradi jinsi Mshirika wa Safari za Google anavyotumia Hotel Center itaendelea kusimamiwa na Sheria na Masharti haya. Ikiwa Mshirika wa Safari za Google atachagua kutumia Huduma fulani za hiari za Hotel Center, basi Mshirika wa Safari za Google huenda atahitajika kukubali kutenganisha masharti ambayo yanahusiana haswa na Huduma hizo.  Baadhi ya Huduma za Hotel Center zinatambuliwa kama “Beta” au vinginevyo zisizotumika au za faragha (“Vipengele vya Beta”).  Mshirika wa Safari za Google haruhusiwi kufichua maelezo yoyote kutoka kwenye au kuhusu Vipengele vya Beta au masharti au kuwepo kwa Vipengele vyovyote vya Beta visivyo vya umma.  Google au Washirika wake wanaweza kusimamisha, kubadilisha au kufunga Huduma kabisa, ikiwa ni pamoja na Vipengele vya Beta, wakati wowote.  Kwa madhumuni ya Masharti haya, “Mshirika” ni huluki yoyote inayodhibiti moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, inayodhibitiwa au hudhibitiwa pamoja na Google mara kwa mara.

 

2. Akaunti.  Ili Mshirika wa Safari za Google atumie Hotel Center, anatakiwa kuwa na Akaunti moja au zaidi zilizofunguliwa na kuidhinishwa na Google.  Ili kuthibitisha Akaunti, mara kwa mara, Google inaweza kuhitaji taarifa za ziada, ikiwa ni pamoja na jina la huluki ya kisheria, huduma ya kibiashara, anwani ya msingi, nambari ya simu, anwani na vikoa vinavyohusika. Mshirika wa Safari za Google anawajibikia matumizi yake ya Hotel Center, ikiwa ni pamoja na matumizi yote ya Akaunti, Maudhui yanayowasilishwa kwa Hotel Center kupitia Akaunti na ulinzi wa majina ya watumiaji na manenosiri ya Akaunti.

 

3. Sera

a. Jinsi Mshirika wa Safari za Google anavyotumia Hotel Center inategemea (i) sera za Google zinazotumika zilizopo katika https://support.google.com/hotelprices/topic/11077677 na sera nyingine zote ambazo Google imempa Mshirika wa Safari za Google, ambazo zinaweza kubadilishwa na Google mara kwa mara (kwa pamoja, “Sera”), (ii) Masharti haya na (iii) jinsi Mshirika wa Safari za Google anavyotii sheria husika. 

b. Kuhusiana na Hotel Center, (i) Google itatii Sera ya Faragha ya Google inayopatikana kwenye google.com/policies/privacy (ambayo itabadilishwa mara kwa mara) na (ii) kwa kiwango kinachowezekana, Google na Mshirika wa Safari za Google wanakubali Sheria na Masharti ya Google kuhusu Ulinzi wa Data ya Mdhibiti kwa Mdhibiti yanayopatikana kwenye https://privacy.google.com/businesses/gdprcontrollerterms/ (“Masharti ya Ulinzi wa Data”).  Google haitabadilisha Sheria na Masharti ya Ulinzi wa Data, isipokuwa kama inavyoruhusiwa wazi chini ya Masharti ya Ulinzi wa Data.

 

4. Maudhui ya Mshirika wa Safari za Google.

a. Mshirika wa Safari za Google anaipa Google leseni isiyoweza kubatilishwa, ya duniani kote, isiyo na mrabaha ya kutumia Maudhui (kwa kiwango kinachokubaliwa na haki za uvumbuzi) kuhusiana na bidhaa na huduma za Google au Washirika wake kwa kipindi kirefu zaidi cha haki hizo za uvumbuzi kinachoruhusiwa chini ya sheria husika. Mshirika wa Safari za Google anakubali kwamba Google inaweza kutoa leseni kwa Washirika na wakandarasi wanaotekeleza huduma za Google, na kwa watumiaji wa Google ili waweze kutumia maudhui kama haya kuhusiana na matumizi ya bidhaa na huduma za Google au Washirika wake.

b. Ikiwa Maudhui yaliyowasilishwa na Mshirika wa Safari yana URL au maudhui sawa na hayo, Mshirika wa Safari anaipa Google haki ya kufikia, kunakili katika faharasa, kuweka akiba au kutambaza URL na maudhui yanayopatikana kupitia URL hizo. (“Maeneo ya Kutembelea”).  Kwa mfano, Google inaweza kutumia programu ya kiotomatiki kuchukua na kuchanganua tovuti zinazohusiana na URL hizo.  Mshirika wa Safari anakubali kwamba maudhui yoyote yanayokusanywa na Google au Washirika wake kutoka Maeneo ya Kutembelea yatachukuliwa kuwa Maudhui na kushughulikiwa kwa mujibu wa Sheria na Masharti haya.

c. Kwa kutumia Hotel Center, Mshirika wa Safari za Google anaidhinisha Google kutumia chapa za biashara, alama za huduma, majina ya biashara, nembo za umiliki, majina ya vikoa na vitambulishi vingine vyovyote vya chanzo au biashara kuhusiana na matumizi ya Maudhui yaliyoidhinishwa ya Google.

 

5. Majaribio.  Mshirika wa Safari za Google anaidhinisha Google na Washirika wake (a) kufanya majaribio mara kwa mara, ambayo yanaweza kuathiri utumiaji wa Huduma na Mshirika wa Safari za Google (ikiwa ni pamoja na inavyohusiana na Maeneo ya Kutembelea, ubora, nafasi, utendakazi, muundo au marekebisho mengine) bila kutuma arifa kwa Mshirika wa Safari za Google (b) kuwezesha uchukuaji na uchanganuzi otomatiki wa, na kuunda vitambulisho vya jaribio ili kufikia, Maeneo ya Kutembelea.

 

6. Dhima.  

a. Kila mhusika anathibitisha kuwa ana uwezo na mamlaka kamili ya kukubali Sheria na Masharti haya.

b. Mshirika wa Safari anawakilisha na kuthibitisha kuwa: 

i. anamiliki, na ataendelea kumiliki, haki za kutoa leseni na vibali vilivyoainishwa katika Kifungu cha Nne; 

ii. hatatoa Maudhui yoyote ambayo yanakiuka Sera, sheria inayotumika au sera zozote za faragha zinazotumika, au kukiuka haki zozote za uvumbuzi za wahusika wengine; 

iii. ana haki na idhini zote zinazohitajika ili kuipa Google taarifa yoyote iliyokusanywa kutoka kwa au kuhusu mtu binafsi ambayo inalindwa chini ya faragha ya data husika au sheria au kanuni za ulinzi wa data; na

iv. maelezo na uidhinishaji uliotolewa na Mshirika wa Safari (ikiwa ni pamoja na ufumbuzi wote muhimu unaohusiana na bidhaa ambao unahitajika ili kuonyesha ofa za Mshirika wa Safari) ni kamili, sahihi na ya sasa, na yataendelea kuwa hivyo.

c. Dhima za wahusika pekee chini ya Sheria na Masharti haya zimefafanuliwa wazi katika Kifungu hiki cha Sita (Dhima). Kwa mujibu wa Kifungu cha 7(b) (Vighairi vya Vikomo), wahusika wanakanusha masharti yote, dhima na masharti mengine ambayo hayajafafanuliwa wazi katika Sheria na Masharti haya (ikiwa ni pamoja na arabuni zisizotajwa za ubora kwa mauzo au ufaafu kwa madhumuni mahususi).

 

7. Kikomo cha Dhima. Katika Kifungu hiki cha Saba (Kikomo cha Dhima), "Dhima" inamaanisha dhima yoyote, iwe chini ya mkataba, sheria za ulegevu (ikiwa ni pamoja na uzembe), au vinginevyo, na kama inaweza kutarajiwa au kuzingatiwa na wahusika au la.

a. Upungufu. Kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria inayotumika na kwa mujibu wa Kifungu cha 7(b) (Vighairi vya Vikomo):

i. hakuna mhusika atakayekuwa na Dhima yoyote inayotokana na au inayohusiana na Sheria na Masharti haya kwa hasara yoyote ya mapato au faida (iwe ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja); au hasara yoyote maalum, isiyo ya moja kwa moja, ya kuambatana au inayotokea baadaye (iwe inaweza kutarajiwa au kuzingatiwa na wahusika katika Tarehe ya Kuanza Kutumika au la); na

ii. dhima ya jumla ya kila mhusika inayotokana au inayohusiana na Sheria na Masharti haya haiwezi kuzidi Pauni £25,000 za Uingereza 

b. Vighairi vya Vikomo. Hakuna chochote katika Sheria na Masharti haya kinachotenga au kuwekea kikomo Dhima ya mhusika yeyote ya:

i. kifo au majeraha ya binafsi yanayotokana na ulegevu wake au ulegevu wa wafanyakazi au waakilishi wake;

ii. ulaghai au uwakilishi wa uongo na kwa ulaghai;

iii. wajibu wake chini ya kifungu cha 8 (Fidia); au 

iv. masuala ambayo yanaifanya Dhima isiweze kutengwa au kuwekewa vikomo chini ya sheria inayotumika.

 

8. Ahadi ya Kulipa.  Kadri inavyoruhusiwa na sheria inayotumika, Mshirika wa Safari za Google atatetea na kuifidia Google, Washirika wake, mawakala na watoa leseni dhidi ya dhima zote, uharibifu, hasara, gharama, ada (pamoja na ada za kisheria) na gharama zinazohusiana na taratibu zozote za kisheria za watu wengine hadi kiwango kinachotokana na, au kinachohusiana na Maudhui ya Mshirika wa Safari za Google, Maeneo ya Kutembelea, matumizi ya Hotel Center, Huduma zake husika au ukiukaji wowote wa Masharti haya unaofanywa na Mshirika wa Safari za Google.

 

9. Kusimamishwa.  Google inahifadhi haki ya kuzuia, kusimamisha au kusitisha (kwa ujumla au sehemu ya) ufikiaji wa Mshirika wa Safari wa, au kutumia, Hotel Center, Huduma au Akaunti baada ya arifa iliyoandikwa (au kwa kutuma arifa ya mapema ya siku 30 ikiwa inahitajika kwa mujibu wa sheria inayotumika) ikiwa: (a) Mshirika wa Safari anakiuka Sheria na Masharti haya, Sera zozote au sheria zinazotumika; (b) Google inahitajika kufanya hivyo ili kutii mahitaji ya kisheria au amri ya mahakama; au (c) Google inaamini kuwa vitendo vya Mshirika wa Safari vinamsababishia madhara au dhima Mshirika mwingine wa Safari, mhusika mwingine au Google. Ikiwa Mshirika wa Safari anaamini ufikiaji wake wa Hotel Center, Huduma au Akaunti umewekewa vikwazo, kusimamishwa au kusitishwa kimakosa, Mshirika wa Safari anapaswa kurejelea mchakato wa rufaa katika Sera. Mshirika wa Safari za Google anaweza kusimamisha Masharti haya wakati wowote kwa kufunga Akaunti yake (zake) na kuacha kutumia Hotel Center.

 

10. Kubadilisha Masharti.  Google inaweza kufanya mabadiliko yasiyo makuu kwenye Masharti haya wakati wowote bila kutuma arifa, lakini Google itatuma arifa ya mapema ya mabadiliko yoyote makuu kwenye Masharti haya. Mabadiliko ya Masharti hayatatumika kurejelea matukio ya awali na yataanza kutumika siku 15 baada ya kuchapisha kwenye ukurasa huu. Hata hivyo, mabadiliko yanayofanywa kwa sababu za kisheria au katika hali za dharura (kama vile kuzuia matumizi mabaya yanayoendelea) yatatekelezwa punde baada ya arifa kutumwa.

 

11. Sheria Inayoongoza; Utatuzi wa Mizozo. Madai yote yanayotokana na au yanayohusiana na Sheria na Masharti haya au Hotel Center yatasimamiwa na sheria ya Uingereza, na wahusika wanakubali mamlaka ya kipekee ya mahakama za Uingereza kuhusiana na mabishano yoyote (ya kimkataba au yasiyo ya kimkataba) yanayohusiana na Sheria na Masharti haya au Hotel Center  .  Ikiwa Mshirika wa Safari za Google yuko katika eneo la mamlaka linalotumika, Mshirika wa Safari za Google pia anaweza kutuma maombi ya kusuluhisha mzozo wake na Google unaotokana na Sheria na Masharti au Hotel Center kupitia upatanisho. Mshirika wa Safari anaweza kupata maelezo zaidi kuhusu wapatanishi ambao Google iko tayari kushirikiana nao na maagizo ya jinsi ya kuomba upatanishohapa. Isipokuwa inavyotakiwa na sheria husika, upatanishi ni wa hiari, na Mshirika wa Safari za Google wala Google hailazimishwi kusuluhisha mizozo kupitia upatanisho.

 

12. Mengineyo. (a) Masharti haya ni makubaliano kamili ya wahusika kuhusiana na maudhui yao na yanachukua nafasi ya makubaliano yoyote ya awali au sambamba kuhusu mada hizo, ikijumuisha Mkataba au Mikataba yoyote ya Leseni ya Maudhui kati ya Google na Mshirika wa Safari za Google kwa maudhui yaliyowasilishwa kwenye Hotel Center baada ya Mshirika wa Safari za Google kukubali Masharti haya. (b) Mshirika wa Safari za Google haruhusiwi kutoa taarifa yoyote kwa umma kuhusu uhusiano unaohusu Masharti haya (isipokuwa panapohitajika kisheria). (c) Isipokuwa kwa marekebisho ya Sheria na Masharti na Google chini ya Kifungu cha 10, marekebisho yoyote ya Sheria na Masharti haya sharti yakubaliwe na pande zote mbili na sharti yataje wazi kuwa yanarekebisha Sheria na Masharti haya. (d) Arifa zote zinazohusu kusimamishwa au kukiuka sharti ziwe zimeandikwa na kutumwa kwa anwani ya Idara ya Sheria ya mhusika huyo mwingine (au ikiwa haijulikani ikiwa mhusika mwingine ana Idara ya Kisheria, basi zitumwe kwa anwani msingi ya mhusika huyo mwingine au anwani nyingine iliyohifadhiwa). Barua pepe ni arifa zilizoandikwa. Anwani ya barua pepe ya arifa zinazotumwa kwa Idara ya Sheria ya Google ni legal-notices@google.com.  Arifa nyingine zote zinazotumwa kwa Mshirika wa Safari za Google zitaandikwa na kutumwa kwenye anwani ya barua pepe inayohusishwa na akaunti ya Mshirika wa Safari za Google.  Arifa nyingine zote zinazotumwa kwa Google zitaandikwa na kutumwa kwa mtu anayejulikana na Mshirika wa Safari za Google katika Google au kwa njia nyingine inayotolewa na Google. Arifa itachukuliwa kuwa imetolewa inapopokelewa, kama inavyothibitishwa kwa maandishi au njia za kielektroniki. Masharti haya ya arifa hayatumiki kwa huduma ya kuwakilisha hati za kisheria, ambayo badala yake inasimamiwa na sheria inayotumika. (e) Hakuna mhusika atakayechukuliwa kuwa ameondoa haki zozote kwa kutotumia (au kwa kuchelewesha kutekeleza) haki zozote chini ya Masharti haya. (f) Iwapo kipengele chochote cha Masharti haya kitapatikana kuwa kisichoweza kutekelezwa, kipengele hicho kitakatizwa na Masharti yatakayosalia yataendelea na kutumika kikamilifu. (g) Mshirika wa Safari za Google hawezi kukabidhi haki au wajibu wowote wake chini ya Masharti haya bila idhini iliyoandikwa mapema na Google.  (h) Hakuna wafaidi wa nje wa Masharti haya. (i) Masharti haya hayajatumika kuunda wakala wowote, ubia, juhudi ya pamoja au uhusiano wa kiajira katika ya wahusika. (j) Vifungu vya 1, 4, 6-9 na 11-12 vitaendelea kutumika baada ya kuisha au kukomeshwa kwa Masharti haya. (k) Hakuna mhusika au Washirika wake wanawajibikia kushindwa au kucheleweshwa kwa utendaji kwa kiwango kinachosababishwa na hali zilizo nje ya udhibiti wake adilifu.